LUMUMBA YAPIGWA NA UMISSETA MBELE YA MKURUGENZI WA MICHEZO WIZARA YA ELIMU
Kikosi cha UMISSETA Unguja |
Katika kujiweka sawa na Mashindano ya Umoja wa Michezo na
Sanaa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) timu ya Kanda ya Unguja imecheza
mchezo wa kirafiki na timu ya Shule ya Lumumba katika Uwanja wa Amaan asubuhi
ambapo timu ya UMISSETA ya Unguja ikafanikiwa kuibuka na Ushindi wa Mabao 3-1.
Mabao ya Kombain ya UMISSETA yamefungwa na Ali Mohd dakika ya
4 na 50, na jengine likifungwa na Iliyasa Suleiman dakika ya 26.
Bao pekee la Lumumba limefungwa na Ali Assaa dakika ya 32.
Kikosi cha Shule ya Lumumba |
Hassan Tawakal Khairallah Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na
Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar akiwasalimia timu
ya UMISSETA Kanda ya Unguja.
Mashindano ya UMISSETA yanatarajiwa kuanza June 6, 2017 huko Butimba Mkoani Mwanza ambapo Zanzibar mwaka huu zitatoa kanda mbili tofauti, Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.
Comments
Post a Comment