MLINZI KINDA WA TAIFA YA JANG’OMBE AJUMUISHWA KWENYE KIKOSI CHA ROLLING STONE
Mlinzi wa kati wa Timu ya Taifa ya Jang’ombe Ali Juma Maarifa
“Mabata” amejumuishwa kwenye kikosi cha kombain ya Mjini Unguja ambacho
kinajiandaa na Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone yanayotarajiwa kufanyika
mwezi July mwaka huu jijini Arusha.
Mabata ni miongoni mwa walinzi wadogo wanaocheza ligi kuu
soka ya Zanzibar lakini shughuli yake uwanjani tofauti na umri wake ambapo
miaka yake chini ya miaka 17 ataungana na wachezaji wengine wa kombain hiyo
inayofundishwa na kocha Mohammed Seif “King”.
Nyota wengine waliyoitwa hivi karibuni kwenye kikosi hicho ni
Ibrahim Abdallah Ali “Mkoko” wa Miembeni ambae hivi karibuni amerejea Visiwani
Zanzibar akitokea mjini Gentil, Gabon katika michuano ya vijana chini ya umri
wa miaka 17 ya AFCON akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania “Serengeti Boys”
baada ya kutolewa kwa kufungwa 1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B
Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, nchini Gabon.
Wengine ni Aley Ali Suleiman “Manula” Mlinda mlango namba
moja wa Miembeni city pamoja na Juma Ali Yussuf “James” wa Villa United.
Mbali ya wachezaji hao wapya waliyoitwa kwenye kikosi hicho
pia kuna nyota wengine wapya waliyobeba ubingwa msimu ulopita wamerejeshwa
kukipa nguvu kikosi hicho.
Wachezaji hao ni Mlinzi wa kushoto wa Black Sailors Muharami
Khamis “Terra” pamoja na mlinzi wa kulia wa KVZ Abdul hamid Salum “Ramos” ambapo
kwasasa kikosi hicho kitakuwa na wachezaji 25 kwa ujumla.
Wachezaji hao wataungana na wale waliyotangazwa awali wiki
mbili zilizopita ambao ni:-
Walinda Mlango Peter Dotto Mashauri (Schalke 04) na Makame
Mkadar Koyo (Huru).
Wachezaji wa ndani ni Hassan Chalii (Kipanga), Abdul-halim
Ameir (King Boys), Shaaban Pandu (Villa United), Idrissa Makame (Villa FC),
Ramadhan Simba (Calypso), Ali Hassan (Uhamiaji), Fahmi Salum (Mlandege), Salum
Omar (Villa United), Yakoub Omar (Jang’ombe Boys) na Mohd Ridhaa (Villa
United).
Wengine ni Mohd Jailan (Chrisc), Makame Masoud (Schalke 04), Mohd
Mussa (Mapembeani), Abrahman Juma (KMKM), Mohd Haji (Jang’ombe Boys), Abdul-hamid
Juma (ZAFSA) na Ibrahim Chafu (Villa FC).
Comments
Post a Comment