MSHAMBULIAJI WA SERENGETI BOYS AJUMUISHWA KATIKA KIKOSI CHA MJINI UNGUJA, ALIPORUDI GABON TU AFCON KOCHA KING AMDAKA, LEO AANZA MAZOEZI NA WENZAKE
Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu
Mkoko” asubuhi ya leo ameungana na wachezaji wa kombain ya Mjini Unguja kwenye
mazoezi katika Uwanja wa Amaan kwa kujiandaa na Mashindano ya Vijana ya Rolling
Stone yanayotarajiwa kuanyika mwezi July mwaka huu jijini Arusha.
Mkoko amerejea Visiwani Zanzibar juzi akitokea mjini Gentil,
Gabon katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya AFCON akiitumikia timu ya Taifa ya
Tanzania “Serengeti Boys” baada ya kutolewa kwa kufungwa 1-0 na Niger katika
mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, nchini Gabon.
Mara baada ya kumaliza mazoezi asubuhi ya leo Mtandao wa
kisanduzenj.blogspot.com umefanya mahojiano na mshambuliaji huyo kwa kuelezea
kujiunga na timu hiyo ya Mjini.
“Nimefurahi kuona kuwa bado Wanzibar na Watanzania wana imani na mimi, nilipowasili tu Zanzibar kutokea Gabon nkapigiwa simu na kocha King nije kujiunga na timu ya Mjini Unguja, nimefurahi sana na leo nimejiunga na wenzangu kwa kujiandaa na mashindano ya Rolling Stone”.
Aidha pia Mtandao huu tukataka kujua kipi alichojifunza
katika Mashindano ya AFCON ambapo Imu ni miongoni mwa vijana wa Tanzania
waliyoweka rikodi kucheza Mashindano hayo.
“Nimejifunza vingi kule, mana nimezidi kuona kuwa mchezaji
ana thamani gani, tulipokelewa vizuri, tukakaa hoteli nzuri, tumekula vyakula
vizuri, tulikuwa tunalindwa, na kubwa zaidi yani kule unathaminiwa kama ni Professional
Player, kuna tofauti kubwa kucheza mashindano yale na haya tuloyazowea, unapata
hela za kusaidia familia yako, kule Kisandu yani wewe acha tu,”.
Alisema Mkoko.
Pia tukazungumza na Kocha Mkuu wa Kombain ya Mjini Unguja
Mohammed Seif “King” ambapo amesema ujio wa Mshambuliaji wa Imu Mkoko umewafurahisha
sana Viongozi wao huku wakiamini watatetea taji lao la Rolling Stone Jijini
Arusha mwezi July, 2017.
“Leo mazoezi tumempokea Imu Mkoko na ujio wake tumefarijika
sana tunaamini atazidi kuleta hamasa kwenye kikosi chetu na kutetea taji letu”.
Alisema kocha King.
Comments
Post a Comment