MUANDISHI WA BOMBA FM APATA BONGE LA SHAVU
Suleiman Ussi Haji “Mido” ambae ni muandishi na mtayarishaji
wa kipindi cha michezo cha SPORTS BOMBA cha Bomba FM amechaguliwa kuwa afisa
Habari wa Kamati ya Soka Ufukweni visiwani Zanzibar.
Mara baada ya Chama cha Soka Visiwani Zanzibar kupata
uanachama wa kudumu wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” wakaitaka Kamati
ya soka la ufukweni kuunda uongozi mpya ambao rasmi kwasasa umewekwa
hadharani.
Uongozi huo ambao unaongozwa na Ali Sharifu “Adolf” ambae ni
Mwenyekiti, Katibu Fahad Khamis, mshika fedha Hassan Ali Mzee, mjumbe Ali Omar
Abdallah huku Muhsin Ali “Kamara” na Mohd Rajab ni washauri wa kamati hiyo
ambapo Afisa Habari ni Suleiman
Ussi Haji “Mido” .
Tayari kamati hiyo imeshapata baraka zote kutoka ZFA taifa na
imepania kuanza rasmi majukumu yake.
Comments
Post a Comment