WADAU WAIJIA JUU RASIMU YA KATIBA YA ZFA, WENGINE WANA HOJI KWANINI MBUNGE AJUWE KUSOMA NA KUANDIKA WAO MPAKA WAWE NA FORM IV?, NA KWANINI IANDIKWE KWA KIENGEREZA?
Baadhi ya wadau wa Soka Visiwani Zanzibar wameijia juu Rasimu
ya awali ya katiba ya ZFA iliyowasilishwa hivi karibuni kwa kusema kuna
vipengele havifai kabisa kuwemo na kwanini katibu na Mwenyekiti wa ZFA Wilaya
awe na elimu kuanzia kidato cha nne wakati huo huo wakihoji kwanini iandikwe
kwa lugha ya Kiengereza wakati wao ni Waswahili na wanatumia lugha yao ya
Kiswahili.
Wakizungumza wakati tofauti na Mtandao huu baadhi ya Viongozi
wa ZFA Wilaya ambao hawakupenda majina yao kutajwa wamesema ni vigumu sana
kupita rasimu hiyo kwani ina mapungufu mengi sana.
“Hii Rasimu ina vichekesho sana tulipoiona tulishtuka, sisi
viongozi ati tuwe na elimu kuanzia Form IV, kisha imeandikwa kwa Kiengereza
wakati sisi ni Waswahili!, si rahisi kupita mazali na sisi ni miongoni mwa
wapitishaji, kwasababu uongozi si kusoma bali uongozi ni kipaji na mapenzi ya
kitu”.
Juzi Jumatatu ya Mei 29, 2017 Kamati ya kuandika upya katiba
ya ZFA chini ya katibu wao Saleh Ali Said iliwasilisha rasimu ya awali kwa
katibu mkuu wa Chama hicho kwenye Afisi ya ZFA iliyopo Aman Mjini Unguja na
sasa inasubiriwa kusambazwa kwa wadau wao kwa ajili ya kupitiwa.
Kwa mujibu wa katiba ya ZFA wadau wao ni Viongozi wa Zfa
wilaya, Vilabu, kamati ya ufundi, kamati ya soka la vijana, kamati ya soka LA
ufukweni, kamati ya watu wenye ulemavu, kamati ya waamuzi na kamati ya soka la
Wanawake ambao wote tayari wameshapatiwa rasimu hiyo.
Lakini bado baadhi ya Wadau hao wana hofu kubwa baada ya
kuona sifa nyingi zimebdilika zikiwemo ya kuwa na Elimu ya Kidato cha nne kwa Katibu
na Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ambapo baadhi yao viongozi hao hawana sifa hiyo.
Mtandao huu ukamtafuta Katibu wa Kamati hiyo ya kuandika upya
katiba ya ZFA Saleh Ali Said ambae pia ni Mwanasheria wa Chama hicho ambapo
amewatoa wasi wasi wadau waliyopata mshtuko mkubwa baada ya kuiona Rasimu hiyo
huku akiwaambia kuwa hiyo ni Rasimu tu na wapitishaji ni wao na ZFA ambapo wao
wamepewa kuiangalia kisha kama ina kasoro watatoa michango yao wapi na wapi
parekebishwe ili ipatikane katiba iliyobora zaidi ambayo inaendana na CAF.
“Mimi nawaambia wasishtuke hiyo ni Rasimu tu, na wao waipitie
na waifahamu vizuri kisha watatoa michango yao, lakini yote ya yote wenye
maamuzi ya mwisho ya kuipitisha hiyo ni ZFA, sisi kamati kazi yetu ndio hiyo
tunasubiri jukumu jengine, na hicho Kiengereza kama hawafahamu tutawasaidia
mana mimi ukiachia kuwa katibu wa kamati hii pia ni Mwanasheria wa ZFA, sasa
tutawatafsiria na pia huko CAF huipeleki katiba kwa Kiswahili, unapeleka Katiba
kwa Kiengereza ukisikia Uganda, Kenya, Msubiji na hata wenzetu Tanzania wote
katiba zao kwa Kiengereza wala si Kiswahili, muhimu palipokuwa hapajafahamika
tutawatfsiria”. Alisema Saleh.
Kamati ya kuandika upya katiba ya ZFA ina wajumbe sita (6) ambao
ni Afan Othman Juma (Mwenyekiti), Saleh Ali Said (Katibu), Othman Ali Hamad
(Msaidizi Katibu), pia yumo Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya soka la
Wanawake (Zanzibar Queens) Nassra Juma na wengine ni Eliud Peter Mvella na Ame
Abdallah Dunia.
Katibu Form iv hawajafika waisome na watoe mapendekezo kisha ndio uyazingatie kujenga katiba mpya iendane na shirikisho la Mpira Africa kuweni makini msiridhishe kila mtu katika hili ndio tunajenga tunajenga tunajenga warudi shule kisha tutakuja kuwapa nafasi
ReplyDeleteni mwanzo mzuri kamati ya katiba nasisi tunaomba nakala tuangalie limeelezwa moja tu hapa la elimu na kushtua walio wengi vipi sifa za viongozi wa juu nao? tupeni tuone tuchangie kisheria sio kibubusa
ReplyDelete