ZU YAONGOZA KUCHEZA FAINALI MARA NYINGI ZAHILFE CUP, KESHO KISASI CHENGINE KWA AFYA, ANGALIA HISTORIA YA TIMU ZILIZOTINGA FAINALI MIAKA YOTE

Fainali ya Mashindano ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar (ZAHILFE CUP) inatarajiwa kusukumwa kesho majira ya saa 10:00 za jioni kwenye uwanja wa Amaan kati ya Mabingwa wa watetezi wa Mashindano hayo Chuo cha Zanzibar Univeristy (ZU) dhidi ya Chuo cha Afya Mbweni.

Historia ya Mashindano hayo ambayo kwasasa ni Mashindano ya 5 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013, ZU ndio timu iliyocheza mara nyingi fainali baada ya kucheza mara 3 na kufungwa mara mbili wakishinda mara 1 ambapo kesho itakuwa fainali yao ya 4 kucheza katika Mashindano hayo.

Bado rikodi zinaonesha kuwa ZU ni Chuo Bora baada ya kufika fainali miaka yote isipokuwa mwaka mmoja (2014) kwenye miaka 5 ya Mashindano hayo.

Afya Mbweni hii ni mara ya pili kufika fainali kufuatia mwaka 2013 kuwafunga ZU bao 1-0 ambapo kesho ZU anataka kulipa kisasi huku Afya wanataka kuendeleza kuwafunga tena fainali ZU.

HISTORIA YA ZAHILFE
2013  AFYA MBWENI PENALTI 5-4 ZU, DAKIKA 90 WALITOKA 0-0
2014 CHWAKA PENALTI 5-4 ZITOD, DAKIKA 90 WALITOKA 1-1
2015 SUMAIT 1-0 ZU 
2016 ZU 4-2 CHWAKA
2017 ZU v/s AFYA?.



Comments

  1. Kimwndishi nikukumbushe mechi ya Sumait na ZU haikufijia matuta kama ulivyoandika bali Sumait ilishinda moja bila goli ambalo lilifungwa mnamo dakika ishirini za kipindi cha kwanza na kudumu hadi mwisho wa mchezo tafadhali hapo rekebisha mkuu.

    ReplyDelete
  2. Mbona mimi sioni kosa apo mechi ya chwaka na zitod ndio ilimaliza kwa penalti na sio ya ZU na SUMMAIT

    ReplyDelete
  3. ZU 3-0 AFYA SISI NI WANAFUNZI WA MWANZO ZU KISANDU 1998 CHINI YA UONGOZI WA PROFFESOR SHAMSHUDEEN

    ReplyDelete
  4. ZITO KABWE ALIPITIA ILA ALIACHA AKAJIUNGA UDSM HAKUMALIZIA DR. ABDALLAH HASNUU MAKAME MBUNGE EA ALIPITIA HAPO Dr. MIRAJI JUNIOR MKURUGENZI MASOKO KAMISHENI YA UTALII WOTE NI MATUNDA YA ZU WA 1998 HAO

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA