BAADA YA KUKAA NJE YA SOKA ZAIDI YA MIAKA 10, KOCHA BURHAN MSOMA AELEZEA KILICHOMREJESHA, APANIA KULETA MABADILIKO YA SOKA LA ZANZIBAR
Kocha wa zamani wa Simba, Kagera Sugar,Nairobi, Kenya Army, Fesal
Sports Club, Forodha, Kikwajuni na Bandari, Burhan Msoma amerejea kwenye soka
na sasa ni kocha mkuu wa klabu ya Gulioni FC inayoshiriki ligi daraja la Pili
Wilaya ya Mjini.
Msoma ambae amefundisha soka kwa mafanikio hasa katika klabu ya
Simba mwaka ya 2004 na kufanikiwa kufika hatua ya Robo fainali ya kwenye
Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika, ametoboa siri ya kurejea tena katika
soka ambapo amesema siri kubwa baada ya kuona soka la Zanzibar limedorora ndipo
alipoamua kurejea baada ya kushawishiwa na Gulioni.
Amesema ameona soka la Zanzibar linazidi kupotea ndipo
aliposhawishiwa na Abdul Mshangama kurejea tena nae akakubali ili akalikombowe
ambapo amepania kulikomboa soka hilo.
“Ni kweli nimekaa miaka mingi sana soka la Zanzibar silitaki
hata kulisikia, lakini sababu kubwa ilonifanya nirejee kufundisha baada ya
kushawishiwa na Abdul Mshangama kwenda kufundisha Gulioni, nikaamua bora nije kulikomboa
soka la Zanzibar mana mbali ya Mshangama kuna wengi wamenishawishi nirudi
katika soka akiwemo ndugu yangu Abdulghan Msoma, Chile na wengine wamenambia
njoo hamasishe soka sasa linarudi katika ubora wake, namimi nikaamua kurudi”.
Timu yake Msoma Gulioni leo saa 10 za jioni itacheza mchezo
wa kirafiki dhidi ya Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini mchezo ambao utasukumwa
katika uwanja wa Amaan.
Mbali na mchezo wa leo pia Gulioni watacheza mchezo mwengine
wa kirafiki sikukuu ya Eid ya Pili dhidi ya Taifa ya Jang’ombe saa 2:00 za
usiku katika uwanja wa Amaan, kisha
kucheza tena sikukuu ya Nne dhidi ya Jang’ombe Boys saa 2:00 za usiku katika
uwanja wa Amaan.
Burhan Msoma |
Comments
Post a Comment