BAZA TAIFA UCHAGUZI JULY 9, WILAYANI JULY 1 NA JULY 4
Chama cha Mpira wa Kikapu Zanzibar (BAZA) kinatarajia kufanya
Uchaguzi wake ambao umepangwa kufanyika July 9, 2017.
Katibu wa kamati ya Uchaguzi Kibabu Haji ametaja ratiba yote
ya uchaguzi ambapo Uchaguzi huo unaanzia Wilayani na July 9 ukifanyika wa
Taifa.
Ratiba ya uchaguzi wa BAZA ngazi ya Taifa na wilaya kama
ifuatavyo:-
Kuanzia tarehe 14.6.2017 lilianza zoezi la Uchukuaji wa fomu
ambapo tarehe 23.6.2017 ni siku ya mwisho ya urejeshaji wa fomu kwa wagombea wakati
wa saa za kazi.
Tarehe 24.6.2017 ni usaili wa wagombea baada ya kuthibitishwa
kuwa mgombea anaruhusiwa kuanza kampeni na pingamizi kwa mgombea.
Tarehe 01.7.2017 uchaguzi Wilaya Mjini ambapo tarehe 04.7.207 ni uchaguzi Wilaya
Chake .
Tarehe 09.7.2017
uchaguzi BAZA Taifa utafanyika Unguja.
Bei ya fomu kugombea
nafasi za uongozi wilaya ni tsh 15,000/= na ngazi ya taifa tsh 40,000/=
NAFASI ZINAZOGOMBANIWA
WILAYA NI:-
MWENYEKITI
MAKAMO MWENYEKITI
KATIBU
MSHIKA FEDHA
MSAIDIZI MSHIKA FEDHA
BAZA TAIFA
MWENYEKITI
MAKAMO MWENYEKITI-PBA
KATIBU MKUU
MSAIDIZI KATIBU-PBA
MSHIKA FEDHA
MSAIDIZI MSHIKA FEDHA-PBA
Comments
Post a Comment