KESHO NI MLANDEGE NA TAIFA MECHI MAALUM YA KUMUAGA NINJA ALIYESAJILIWA YANGA
KESHO Ijumaa ya June 23, 2017 Saa 3:00 za usiku katika Uwanja
wa Amaan Mlinzi mpya wa Yanga Abdallah Haji Shaibu "Ninja" atawaaga
Mashabiki wake katika mchezo maalum kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi Mlandege
SC mchezo ambao pia ni wa uzinduzi wa COCO SPORTS NDONDO CUP.
Ninja amesajiliwa Yanga wiki iliyopita akitokea Taifa ya
Jang’ombe ya Zanzibar ambapo amefunga mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu
hiyo na kesho atapata fursa kubwa ya kuwaaga Mashabiki wake.
Kiingilio katika mchezo huo ni Shilingi Elfu 2000/=,
3000/= na VIP 5000/=.
|
Comments
Post a Comment