HUYU MLINZI KINDA HATARI WA REAL KIDS, JANA KAKABA ULINZI TAIFA NOWMA, SAMIR AMPA TANO
Zanzibar ni Visiwa vyenye vipaji vingi sana ambapo kila siku
vinaibuka vyengine vipya, tukija kwenye soka sitaki kuongea sana lakini jana
kama umeangalia mchezo wa kirafiki kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Gulioni katika
uwanja wa Amaan, bila ya shaka umemuona kinda jipya limefunga mlango kwenye
safu ya ulinzi ya Taifa, si mwengine bali ni Ibrahim Abdallah ni beki wa kati
wa timu ya Real Kids inayoshiriki ligi za madaraja ya vijana wilaya ya Mjini,
lakini jana alitumiwa na Taifa na alivaa jezi nambari 29 mgongoni.
Ibrahim unaweza ukamuona ni mlinzi wa kawaida lakini huyu
dogo ni nowma hata Samir Yahya beki wa kati wa Taifa ya Jang’ombe amekubali
kazi yake jana na kusema huyu mtoto hatari.
“Nime enjoy sana leo kucheza na Ibra katikati, dogo ana
kibaji na anauwezo, anakuja vizuri sana naamini akizidi kucheza atakuwa bonge
la beki hapa Zanzibar, nimefurahi sana na huwenda akawa mrithi wa Ninja au hata
mimi nikiondoka basi naamini dogo ataziba pengo bila ya wasi wasi, kuna vitu
vidogo tu vinarekebishika”. Alisema Samir beki wa Taifa.
Lakini yote 9, kumi wale walopata fursa ya kuangalia Mashindano
ya Michezo na Sanaa ya Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA), mashindano
ambayo yalimalizika hivi karibuni katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba
huko mkoani Mwanza unaambiwa beki huyo alikuwa gumzo sana huko Mwanza, kama
ulisikia Timu ya Unguja ilicheza zaidi ya mechi 4 bila ya kuruhusu kufungwa
hata bao 1, basi kazi ya mlinzi huyo ilitendeka.
Mlinzi huyo yupo kwenye majaribio ya mwisho kujiunga na Taifa
ya Jang’ombe ili kuziba pengo la Abdallah Haji Shaibu “Ninja” aliyesajiliwa
Yanga pamoja na kuziba nafasi ya Ali Juma Maarifa “Mabata” ambae anatarajiwa
kwenda Mkoani Manyara katika Mashindano ya Rolling Stone baada ya kuitwa kwenye
Kombain ya Mjini Unguja.
Mtandao huu unamtakia kila la kheir mlinzi huyo Ibrahim Mungu
amlinde kipaji chake.
Ibrahim Abdallah (Kushoto) na Samir Yahya (Kulia) |
Comments
Post a Comment