BOYS YABANWA NA WATOTO WA MJINI, WATAKIPIGA TENA LEO JIONI NA GULIONI
Timu ya Soka ya Kombain ya Wilaya ya Mjini na Jang'ombe Boys zimeshindwa
kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0 katika mchezo maalum wa kirafiki
uliosukumwa jana
Jumatano saa 3 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Mjini watacheza mchezo mwengine wa kirafiki leo Alhamis
kuanzia saa 10:15 za jioni dhidi ya timu ya Gulioni ambayo inashiriki ligi
daraja la Pili Wilaya ya Mjini.
Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja kwa majukwaa
ya kawaida na V.I.P ni shilingi Elfu mbili.
Kombain ya Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Rolling Stone
yanayotarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017 huko Mburu Manyara wakati
Jang'ombe boys wanajiandaa na kuendelea kucheza hatua ya 8 bora ligi kuu soka
ya Zanzibar.
Kikosi cha Gulioni |
Comments
Post a Comment