CHARAWE WAKANUSHA KUUZA DARAJA, WASEMA HATA WAPEWE MILIONI 200 TIMU HAWAITOWI LENGO LAO KUCHEZA LIGI KUU NA KUCHUKUA UBINGWA
Uongozi wa klabu ya Charawe Stars umekanusha taarifa za kuuza
daraja kwa timu yao na kusema kuwa taarifa hizo si kweli na wao wapo katika
maandalizi ya kucheza ligi kuu soka ya Zanzibar msimu ujao.
Akizungumza na Mtandao huu
Ramadhan Abdallah “Sadifa” ambae ni msemaji wa timu hiyo amesema taarifa
zilizozagaa mitaani ya kuwa timu yao imeuzwa sio kweli na kamwe hawawezi
kufanya jambo hilo kwani ile ni timu ya Kijiji na lengo lao kucheza ligi kuu
ndio mana wakapigana kufika hapo walipo.
“Hizo taarifa sio kweli timu yetu hatuuzi wala haitouzwa,
sisi tupo kwaajili ya kupambana kucheza ligi kuu ya Zanzibar, tunashukuru
tumefanikiwa kutoka daraja la kwanza na kufika hapo tulipo kwasasa tunasubiri
ligi kuu kucheza, hiyo timu inayosema inataka kununuwa nafsi yetu hata watuletee
million 200 hatukubali, sisi tumepigana ndo mana tukafika ligi kuu na wao kama
rahisi wapigane, sisi sio genge hii ni timu ya Wanakijiji, kama rahisi nawao
wapigane wafike hapa tulipofika sisi, msimamo wetu timu hatuitowi hata waje na
pesa gani tunataka kucheza ligi kuu ya Zanzibar na kubeba kombe” Alisema Sadifa.
Hivi karibuni kumeibuka tetesi nyingi zinazosema timu ya
Mlandege SC wamenunuwa daraja la Charawe hivyo taarifa hizo za kukanusa msemaji
wa Charawe zitawasaidia kujua watu wengi ambao waliyofikiria kuwa kweli timu ya
Charawe imeuzwa.
Comments
Post a Comment