GULIONI WANAKUJA KIVYENGINE MSIMU HUU, KWANZA WANAANZA NA TAIFA KISHA BOYS
Timu ya Soka ya Gulioni FC inayoshiriki ligi daraja la Pili
Wilaya ya Mjini imepania kuwatia michezo miwili ya kirafiki kwenye sherehe za
Sikuu ya Eid pili na nne ambapo Eid Pili watasukumana na Taifa ya Jang’ombe
kisha Eid nne kucheza na Jang’ombe boys mechi zote zitachezwa saa 2:00 za usiku
katika Uwanja wa Amaan.
Akizungumza na Mtandao huu Rais wa Gulioni Ahmed Khamis
amesema maandalizi ya michezo hiyo yanaendelea vizuri na lengo lao ni kufanya
mapinduzi ya soka la Zanzibar.
“Tumejiandaa vizuri kucheza na Taifa Eid pili kisha Boys Eid
nne lakini sisi lengo letu ni kuleta mapinduzi ya soka la Zanzibar”. Alisema
Ahmed.
Comments
Post a Comment