JKU ACADEMY YAPANIA KUCHUKUA UBINGWA WA ROLLING STONE, MAPEMA WANATANGULIA ARUSHA KUZOWEA BARIDI
Timu za JKU Academy zimepania kubeba ubingwa wa Mashindano ya
Vijana ya Afrika Mashariki na Kati (Rolling Stone) ambapo mwaka huu wakitarajia
kushiriki timu tatu tofauti katika Mashindano hayo ikiwemo timu chini ya miaka
13, 15 na 17 ambapo msafara wa watu 60 ukitarajiwa kuondoka Visiwani Zanzibar
Jumapili usiku July 2, 2017.
Msafara huo ambao utajumuisha timu tatu tofauti za JKU
Academy pamoja na waamuzi wao vijana watano na viongozi watano.
Mtandao huu umemtafuta Khatib Omar Salum ambae ni kocha mkuu
wa JKU Academy na ametuelezea mchakato mzima wa safari yao kwenda huko na
maandalizi yao walivyojipanga.
“Jumapili tunatarajia kuondoka Zanzibar, tunategemea Jumatatu
tuanze safari ya Arusha na tutafika Jumatatu usiku, tunaenda mapema ili tuzowee
mazingira ya baridi lakini pia mimi naamini tutabeba vikombe mwaka huu, tuna
timu tatu n azote zipo vizuri sana mwaka huu”. Alisema.
Mashindano ya Rolling Stone mwaka huu yanatarajiwa kuanza
rasmi July 9 na kumalizika July 19, 2017 ambapo msimu huu kumepangwa vituo
tofauti makundi mengine yamepangiwa Arusha, mengine Manyara.
Comments
Post a Comment