KESHO NI ZAMU YA BOYS NA GULIONI SHEREHE ZA KUFUNGA SIKUKUU ZA EID
Kikosi cha Gulion FC |
Timu ya Gulioni FC bado inaendelea na mchakato wake wa
kujiweka sawa kucheza ligi Daraja la Kwanza Taifa Unguja msimu mpya ambapo
kesho Alhamis Iddi nne watacheza mchezo mwengine wa kirafiki na timu ya Jang’ombe
boys, mchezo ambao utasukumwa saa 2:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan.
Gulioni jana walipigwa 2-1 na Taifa ya Jang’ombe katika
mchezo wa kirafiki ambapo kesho wamepania kufuta makosa yao mbele ya Boys.
Viingilio vya mchezo huo ni Shilingi 2000/=, 3000/= na VIP 5000/= .
Kikosi cha Jang'ombe Boys |
Comments
Post a Comment