“KILA MTU ANAWEZA NA HAKUNA KUKATA TAMAA HATA WAZANZIBAR WANAWEZA KUCHEZA LIVERPOOL” - MAMADOU SAKHO
Sakho na watoto wake akiwa pamoja na mmiliki wa blog hii Abubakar Khatib (Kisandu) |
Katika Maisha hakuna kukata tamaa hasa kwa Vijana kwani hakuna
kisichowezekana katika Dunia hii, hayo si maneno yangu bali ni maneno ya beki
wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England wakati
alipokuwa akiangalia mpira katika Visiwani Zanzibar katika Uwanja wa Aman kwenye
mchezo maalum wa uzinduzi wa COCO SPORTS NDONDO CUP ambapo Taifa ya Jang’ombe
walipigwa 2-1 na Mlandege.
Amesema ni kosa kwa kijana kukata tamaa kwani akiweka malengo
na kujituma atatimiza ndoto zake.
“Ukiwa na malengo kisha ukajituma zaidi basi unaweza kutimiza
ndoto zako, kwa wachezaji wa hapa Zanzibar hata Liverpool wanaweza kucheza
lakini wakiwa na malengo yao na kujituma, hakuna kisichowezekana, mimi napenda
kuona vijana hawakati tamaa”.
Aidha Sakho amefurahishwa mno katika mchezo huo kwenye uwanja
wa Amaan huku akisema kuwa ame enjoy sana mapumziko yake Visiwani Zanzibar huku
akisema mchezaji yoyote anaweza kucheza Ulaya.
“Nime enjoy sana Zanzibar, uwanjani mashabiki wengi
wamenipokea kwa furaha na mimi nijisikia furaha sana, kuhusu wachezaji wa
Zanzibar nimewaona lakini mimi maneno yangu ni yale yale, watu wote wanaweza
kufanya lolote na kufika popote”.
Sakho ataondoka leo Saa 8 za mchana katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Abeid Amani Karume na kurejea nyumbani Ufaransa ambapo alikuwepo
Visiwani Zanzibar na familia yake tangu Jumamosi ya June 17, 2017 kwa ziara ya
kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani
Ufaransa na badae moja kwa moja kufika hapa Zenj.
Comments
Post a Comment