KLABU YA KOREA KUCHEZA NA TAIFA YA JANG’OMBE
Kikosi cha Hallelujah FC |
Klabu ya Halelujah FC inayoshiriki ligi daraja la Pili Korea
ya kusini kesho Jumamosi July 1, 2017 itacheza mchezo wa kirafiki na timu ya
Taifa ya Jang’ombe ambayo inashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar, mchezo huo
utapigwa majira ya saa 9:30 ya Alaasir katika uwanja wa Amaan.
Katika mchezo huo hakutokuwa na kiingilio chochote ambapo
Wakorea wenyewe watatoa tiketi bure kwa mashabiki wote watakaofika Uwanjani
hapo.
Mchezo mwengine wa kirafiki timu ya Halelujah FC itacheza na
timu ya Polisi ya Zanzibar inayoshiriki ligi kuu, mchezo ambao utasukumwa
Jumanne July 4, 2017 saa 9:30 Alaasir katika uwanja wa Amaan.
Hallelujah FC imeanzishwa December 20, 1980 huko kwao Korea
ya Kusini ambapo jana waliwasili hapa Visiwani Zanzibar kwaajili ya kufanya ziara
maalum pamoja na kupata mazoezi kwa kucheza na baadhi ya vilabu vya Zanzibar.
Kikosi cha Taifa ya Jang'ombe |
Comments
Post a Comment