KOMBAIN YA MJINI KUKIPIGA NA JANG'OMBE BOYS
Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini inatarajia kucheza mchezo
wa kirafiki na Jang'ombe Boys kesho kutwa Jumatano saa 3 za usiku katika uwanja
wa Amaan.
Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja na V.I.P ni
shilingi Elfu mbili.
Kombain ya Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Rolling Stone
yanayotarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017 huko Mburu Manyara wakati
Jang'ombe boys wanajiandaa na kuendelea kucheza hatua ya 8 bora ligi kuu soka
ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment