MAJESHI WA TANZANIA WAPANIA KUFANYA KWELI MASHINDANO YA MAJESHI YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
Timu za michezo mbali mbali za Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) zimepania kutwaa ubingwa katika Mashindano ya Majeshi ya Afrika
Mashariki na Kati Mashindano ambayo mwaka huu yatafanyika Bujumbura Mjini
Burundi mwanzoni mwa mwezi Agost.
Akizungumza na Mtandao huu Kanal Mwandike ambae ni Mkurugenzi
wa Michezo wa JWTZ amesema wamepania kufanya kweli mwaka huu ambapo matayarisho
ya Mashindano hayo yanaendelea vizuri na sasa wapo kambi Visiwani Zanzibar kwa
kujiandaa na Mashindano hayo.
Amesema lengo lao mwaka huu kubeba kombe hilo ambapo mwaka
jana walichukua nafasi ya pili katika Mashindano hayo.
“Mwaka huu tumepania kufanya vyema kuliko mwaka jana, mana
mwaka jana tulishinda nafasi ya pili, tupo hapa Zanzibar kwaajili ya Maandalizi
na tumepania kufanya kweli mwaka huu”. Alisema Kanal Mwandike.
Mashindano ya Majeshi ya Afrika Mashariki na Kati hufanyika
kila mwaka, ambapo mwaka huu Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litashiriki
kwa michezo mitano ikiwemo mpira wa Miguu, mpira wa Kikapu, mpira wa Wavu,
mpira wa Pete na Riadha.
Comments
Post a Comment