MAMADOU SAKHO- “BABAANGU ALIKUFA NIKIWA NA MIAKA 12 NA MAISHA YALIKUWA MAGUMU MNO, SASA NINA UWEZO NA MUNGU ATANIULIZA PESA ZANGU NIMEZITUMIA VIPI? LAZIMA NIWASAIDIE WANYONGE
Sakho na familia yake wakipiga picha ya pamoja na watoto yatima wa SOS |
Leo Saa 8 za mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume ataondoka Beki wa kimataifa wa Ufaransa na kurejea nyumbani,
Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England ambae alikuwepo Visiwani
Zanzibar tangu Jumamosi ya June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali
ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja
kwa moja kufika hapa Zenj.
Lakini mchezaji huyo anaondoka Zanzibar kwa kuwacha ujumbe
mzito kwa Wazanzibar baada ya kusema kuwa yeye ni tajiri na anauwezo mkubwa
sana lakini binafsi yake anajua fika kuwa akifariki Mwenyezi Mungu atamuuliza
utajiri wake ameutumia vipi?
Amesema yeye anauwezo mkubwa wa fedha na muumini wa Dini ya
Kiislamu hivyo Mungu atamuuliza fedha zake amezitumia kwa njia gani.
“Mimi fedha ninazo nyingi sana na lakini najua fika kuwa
Mungu ataniuliza nimezitumiaje fedha zangu!, nitamjibu vipi nimehonga
wanawake!, hapana hivyo lazima nitowe sadaka kwa kuwasaidia watoto Yatima na
Masikini na ndio maana nina taasisi yangu maalumu ya kusaidia Mayatima na
Masikini”.
Wakati huo huo kumbe Sakho nae alikuwa mtoto yatima na
aliishi maisha magumu sana wakati yupo mdogo na anajua umuhimu wa kuwasaidia
mayatima ndio maana juzi akaenda kuwasaidia watoto Yatima wa kituo cha SOS
Zanzibar.
Baadhi ya vyakula alivyotowa Sakho kwa Watoto Yatima |
“Mimi babaangu mzazi alifariki nikiwa na miaka 12, nilikuwa
mdogo sana na maisha yangu yalikuwa magumu sana, napenda kuwauliza wanangu AIDA
(ana miaka 4) na SIENNA (ana miaka 2) mumezaliwa babaenu anaouwezo mkubwa wa
mali kwaiyo na nyinyi mukiwa wakubwa fedha zenu mutafanya nini, basi
wananiambia watasaidia masikini na Mayatima, nafurahi sana nikiwasikia hivyo na
mimi nazidi kuwasisitiza wawasaidie”.
Sakho alikuwepo Zanzibar pamoja na mke wake anaitwa Majda
ambae ana asili ya Moroco pamoja na watoto wao wawili wote wanawake ambao ni AIDA
na SIENNA waliozaliwa mwaka 2013 na
2015.
Comments
Post a Comment