MWINYI HAJI- BADO KIDOGO NIJIUNGE NA SIMBA LAKINI MAPENZI YANGU NA JANGWANI NDIO YALOSABABISHA NIBAKIE YANGA
Baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea
kukipiga na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga, mlinzi wa kushoto Mwinyi Haji Ngwali
“Bagawai” ametoboa siri iliyomfanya kubakia Jangwani na kutokwenda Msimbazi
licha ya kufatwa na Simba.
Mwinyi amekiri kuongeza mkataba wa miaka miwili Yanga na pia
aliweka wazi kuwa Simba walihitaji huduma yake lakini mapenzi yake Jangwani
ndio sababu kubwa iliyomfanya kubakia Yanga.
“Nimeongeza mkataba wa miaka 2 pale Yanga, na kweli Simba
walinihitaji na mazungumzo yalikuwa yameshaanza na yamefikia pazuri sana,
lakini bado naipenda Yanga yangu ndio mana nimebakia Jangwani”. Alisema Mwinyi.
Comments
Post a Comment