NINJA WA YANGA AWAAGA WAZANZIBAR, ATOA MANENO MAZITO KATIKA UWANJA WA AMAAN
Mlinzi mpya wa Yanga Abdallah Haji Shaibu "Ninja" amewaaga
mashabiki wa soka Visiwani Zanzibar na kuwaomba wamsamehe kama aliwakosea kwa
kipindi chote alichocheza soka Visiwani hapa.
Akiwaaga Mashabiki hao jana usiku katika uwanja wa Amaan
kwenye mchezo maalum wa uzinduzi wa COCO SPORTS NDONDO CUP ambapo Taifa ya Jang’ombe
walipigwa 2-1 na Mlandege, Ninja amewashukuru Makocha wake wote tangu alipokuwa
mdogo mpaka kufika Taifa ya Jang’ombe.
Aidha Ninja amewaomba Mashabiki hao wamsamehe kama aliwakosea
kwa kipindi chote huku akiwataka wazidi kumuombe dua ili afanikiwe katika
Maisha yake mapya ya Jangwani.
“Kwanza Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kusajiliwa Yanga, la
pili na nawashukuru Makocha wangu wote tangu walonifundisha kuanzia Juvenile, Junior
na Central, la tatu nawashukuru Mashabiki wangu wa Taifa ya Jang’ombe kwa
kunisapoti, na pia nawaomba Wazanzibar kama kuna mtu nimemkosea anisamehe na
mimi nimeshawasamehe wote, hivyo muniombe pia dua kwa Mungu anisaidie kwani
lengo langu si kucheza Yanga bali kucheza nje ya Tanzania”. Alisema Ninja.
Ninja ndie mchezaji wa kwanza msimu huu wa mwaka 2017-2018 kusajiliwa
Yanga akitokea Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar ambapo amefunga mkataba wa miaka
miwili kuitumikia klabu hiyo.
Comments
Post a Comment