SAKHO WA LIVERPOOL ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA ZANZIBAR
Familia ya beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England jioni ya leo ametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS kilichopo Mombasa Unguja.
Sakho amefatana na mke wake Madna na Watoto wake wawili wa kike.
Leo Ijumaa saa 3:00 za usiku katika uwanja wa Amaan Sakho atazindua Mashindano ya COCO SPORTS NDONDO CUP katika uwanja wa Amaan, mchezo ambao watasukumana kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Mlandege SC.
Sakho yupo hapa Viswani Zanzibar tangu Jumamosi June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja Jumamosi kufika hapa Zenj.
Comments
Post a Comment