SAKHO WA LIVERPOOL KUZINDUA NDONDO CUP YA COCONUT KESHO IJUMAA KATI YA TAIFA YA JANG'OMBE DHIDI YA MLANDEGE
Beki wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England kesho Ijumaa saa 3:00 za usiku katika uwanja wa Amaan atazindua Mashindano ya COCO SPORTS NDONDO CUP katika uwanja wa Amaan, mchezo ambao watasukumana kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Mlandege SC.
Sakho yupo hapa Viswani Zanzibar tangu Jumamosi June 17, 2017 kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja Jumamosi kufika hapa Zenj.
Sakho amecheza mechi zaidi ya 200 katika klabu hiyo, akishinda nayo mataji yote manne ya nyumbani kabla ya mwaka 2013 kuuzwa Liverpool kwa dau la Pauni Milioni 18.
Mwaka huu alitolewa kwa mkopo Crystal Palace pia ya Ligi Kuu England ambako amekwenda kucheza mechi nane.
Sakho ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha wakubwa cha Ufaransa, ambaye awali amechezea timu zote za vijana na za nchi hiyo.
Tangu acheze mechi yake ya kwanza kikosi cha wakubwa cha Ufaransa mwaka 2010 dhidi ya England, Sakho amecheza mechi zaidi ya 25 na alikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Mke wa Sakho anaitwa Majda, ambaye amezaa naye watoto wawili wa kike, waliozaliwa mwaka 2013 na 2015.
Sakho alizaliwa Februari 13, mwaka 1990, kisoka aliianzia Paris FC kabla ya kuhamia timu ya vijana ya Paris Saint-Germain mwaka 2002 na Oktoba mwaka 2007 aliweka rekodi ya mchezaji kijana daima kuiongoza timu hiyo kam Nahodha katika Ligue 1.
Good inapendeza saana, pia hongera kwenu COCONUT FM, kiukweli sasa mpira unakuwa kwa kiwango kikubwa saana, big up kwenu COCONUT FM
ReplyDelete