SEIFU TIOTE AWAOMBA WADAU WA SOKA KUISADIA KOMBAIN YA MJINI
Kiungo
mshambuliaji wa Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini Seifu Said Seifu (Tiote) amewaomba
wadau wa soka Visiwani Zanzibar kuichangia timu yao ili wafanikishe safari yao
ya kwenda Mburu Mkoani Manyara kushiriki Mashindano ya Vijana ya Afrika
Mashariki na Kati ya Rolling Stone.
Tiote ameyasema
hayo wakati anazungumza na Mtandao asubuhi ya leo huku akisema mazoezi
yanaendelea vizuri na wao wachezaji wana hamasa kubwa sana ya kutetea taji lao
lakini wadau wa soka waisaidie timu yao ili ifanye vizuri kama msimu ulopita.
“Mazoezi
tunaendelea vizuri tuna hamasa kubwa sana mana tunakuja kwa wakati na tunapokea
vizuri mafunzo ya walimu wetu lakini nawaomba wadau wa soka Zanzibar watuunge
mkono kwa kutusaidia chochote ili tuweze kutetea taji mana hii timu
inawakilisha Zanzibar nzima sasa”. Alisema Tiote.
Mashindano
ya Rolling Stone mwaka huu yatafanyika Mikoa miwili tofauti Arusha na Manyara
kuanzia July 9 hadi July 19, 2017 ambapo kundi la Mjini Unguja ambao ndio
mabingwa watetezi limepangwa kuchezwa Manyara.
Seifu Said Seifu (Tiote) |
Comments
Post a Comment