TAIFA YAJIFARIJI SIKUKUU KWA GULIONI
Timu ya Taifa ya Jang'ombe imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gulioni katika mchezo maalum wa kirafiki uliosukumwa leo saa 3 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Mabao ya Taifa yamefungwa na Omar Chande na Adam Ibrahim "Edo" wakati bao pekee la Gulioni limefungwa na Amour Pwina.
Gulioni wanatarajia kucheza mchezo mwengine wa kirafiki siku ya Alhamis Iddi Nne dhidi ya Jang'ombe boys saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Comments
Post a Comment