WALORATIBU SAFARI YA SAKHO WA LIVERPOOL ZANZIBAR 3:00 ZA ASUBUHI WATAZUNGUMZA NA COCONUT FM KUHUSU SAKHO KUFIKA AMAN LEO
Kampuni ya Escapade Zanzibar Limited ambayo ndio Kampuni
iliyompokea na kusimamia shughuli zote za ziara ya Nyota wa kimataifa wa
Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England, Kampuni hiyo
itazungumza na Coconut FM 88.9 leo kuanzia saa 3:00 za asubuhi na kumuelezea
mchezaji huyo kuhusu ujio wake wa kwenda kuzindua Mashindano ya COCO SPORTS
NDONDO CUP katika uwanja wa Amaan, mchezo ambao watasukumana kati ya Taifa ya
Jang’ombe dhidi ya Mlandege SC leo kuanzia saa 3:00 za usiku.
Sakho yupo hapa Viswani Zanzibar tangu Jumamosi June 17, 2017
kwa ziara ya kiutalii ambapo awali ziara hiyo alianzia Tanzania bara kisha
kurejea nyumbani Ufaransa na badae moja kwa moja Jumamosi kufika hapa Zenj.
Wapenzi wa soka watakaofika katika Uwanja wa Amani leo
watapata fursa ya kumuona na wengine kupiga nae picha nyota huyo.
Vingilio ni:-
Tsh 2000 urusi
Tsh 3000 wings
Tsh 5000 V.I.P
Comments
Post a Comment