WAZANZIBAR WENGINE 2 KUTAKA KUSAJILIWA LIGI KUU BARA
Kocha mkuu wa timu ya Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali
Bushir “Bush” amepania kufanya usajili wa wachezaji wa nne wapya kwa nafasi
tofauti wakiwemo Wazanzibar wawili.
Bushir amesema amepania kusajili wachezaji wa nne akiwemo Mlinda
Mlango na Kiungo mkabaji kutoka Ligi kuu soka ya Zanzibar na wengine wawili ni
Kiungo mshambuliaji na Mshambuliaji wa kati kutoka Ligi kuu soka ya Tanzania
Bara.
Amesema tayari ameshaanza mazungumzo na Wachezaji hao lakini
kwasasa bado hajaweka wazi majina yao.
“Nimepania kusajili wachezaji 4 tu katika dirisha hili,
nafanya hivyo kwa vile wachezaji wangu wengi wameshanifahamu vyema taaluma yangu
ndo mana ntasajili wa nne tu ili kuja kuongezea nguvu tu, wachezaji ambao
nimeshaongea nao ni mlinda mlango na kiungo mkabaji kutoka ligi kuu ya
Zanzibar, na wengine ni kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wa kati mmoja hawa
wote kutoka ligi kuu ya bara, majina kwasasa sitowataja kwa vile nishapeleka
ripoti kwa uongozi na binafsi nimeshaongea nao, Zanzibar kuna vipaji vingi sana
nawaomba vijana wazidi kujituma ili wapate nafasi ya kucheza nje ya Zanzibar na
hata timu ya Taifa tutakuwa nayo nzuri ukiangalia na sasa sisi Zanzibar ni
wanachama wa CAF”. Alisema Bushir.
Kocha Bushir alitokea KMKM ya Zanzibar na alijiunga na Mwadui FC msimu ulopita katika
dirisha dogo na kufanikiwa kumaliza nafasi ya 10 katika ligi hiyo ambapo
aliichukua timu hiyo ikiwa ipo nafasi ya 15 nafasi ambayo ni ya pili kutoka
mkiani.
Ali Bushir |
Comments
Post a Comment