ZAIDI YA MAKOCHA 30 KUSHIRIKI KOZI YA MAGOLIKIPA ZANZIBAR
Mkufunzi Saleh Ahmed Seif "Machupa" |
Kozi ya awali ya makocha wa Magilikipa Visiwani Zanzibar
inatarajiwa kufanyika July 5 na kumalizika July 11, 2017 chini ya Mkufunzi
Gwiji Saleh Ahmed Seif “Machupa”.
Kozi hiyo imeandaliwa na Chama cha Soka Zanzibar “ZFA” ambayo
itawashirikisha zaidi ya makocha 30 kutoka Unguja na Pemba na makocha hao wakimaliza
kozi hiyo watapata fursa ya kutambuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF”.
Mtandao huu umemtafuta Mkufunzi huyo Machupa na kutaka kujua
matayarisho yanaendeleaje ya Kozi hiyo ambapo amesema kila kitu kipo sawa mpaka
sasa na yeye baada ya kuhitimu kozi ya Ukufunzi aliagizwa na CAF kuendesha kozi
popote nchini Tanzania.
“Matayarisho yanaendelea vizuri mpaka sasa, mimi niliagizwa
na CAF niendeshe kozi kama hizi maana makocha wengi wanafundisha lakini hawana
taaluma ya ukocha wa makipa”. Alisema Machupa.
Machupa ni Mkufunzi pekee nchini Tanzania aliyehitimu Kozi ya
CAF ya Wakufunzi wa Makocha wa Magolikipa wa ndani kozi ambayo aliisomea nchini
Cameroon mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu, Machupa pia ameshahitimu kozi ya FIFA ya
Ukocha wa Magolikipa ya hatua ya juu (Advanced Level) ambayo aliipata kwenye
kozi iliyofayika tarehe 01 Agost, 2016 na kumalizika tarehe 05 Agost 2016, na
pia Machupa ana Leseni “B” ya Ukocha inayotambuliwa na CAF.
Comments
Post a Comment