BUSHIR NDO BASI TENA MWADUI FC, AONDOKA NA UJUMBE MZITO
Kocha mkuu wa Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga Ali Bushir “Bush”
amefutwa rasmi kazi kuwa kocha wa timu hiyo baada ya kuongoza
timu hiyo kwa nusu msimu na kuisaidia kubakia kwenye ligi kuu soka Tanzania
bara.
Taarifa hizo tumezithibitisha kupitia ukurasa wake mwenyewe
mwalimu huyo wa Facebook ambao ameandika kuwa amefutwa rasmi kazi huku pia
akielezea sababu iliyopelekea kuondoshwa.
“Shortlly ni kua NIMEFUTWA rasmi kazi ya kua kocha Mkuu wa
timu ya Mwadui Fc kwa kipindi kifupi cha nusu mwaka nlokua nkiihudumikia.
Ukweli hakuna Mtz hata mmoja ambae ni mdau wa soka ndani ya nchi yetu asiyejua
ni kwa vp nliisaidia timu hio ktk kazi ambayo walinichukulia kuifanyia timu
hiyo na naam niliifanya na lkn c kwa ujanja wng tuu bali na Mungu alinisaidia
ktk kuifanikisha kazi hio.. Kuna v2 v3 ambavyo viliniponza hadi kufikia
kuipoteza kazi yng hio.. La kwanza ni haki zangu {financially} la pili ni kuusu
usajili na la tatu ni kuusiana na chuki na choyo kutoka kwa asst nliyekua nae
vl yy ndo nlomkuta pale.. So Paaalllsss kwa maelezo yng zaidi bc fwatilieni
magazeti ya kesho vl kuna gazeti la michezo mtaikuta story hio.. Lkn all above
all mii c mwalimu mkuu tena wa Mwadui fc”. Aliandika katika ukurasa wa Facebook.
“Any way! Who knows? Jst wait n c ni wapi ntakoelekea
hukohuko ktk ligi kuu ya Vodacom na Inshllh ntawajulisha tuu Paaallllssss wngu,
vl taari nshapata mialiko kadhaa ila tuu bado cjaamua ni wapi nielekee..
Paaalllss nimeamua kuwaambia ukweli wng ktk hili ili tuu mcsikilize ya wa2
mitaani vl ukweli ni huo.. Gd9t Paaaalllss...!!!!”.
Katikati ya msimu uliopita Bushir alichukua mikoba ya Jamhuri Kihwelo
‘Julio’ na kujiunga na Mwadui FC ambapo aliikuta timu hiyo ipo nafasi ya tatu
kutoka chini na kufanya kazi kubwa mpaka kuisadia kuinusuru kushuka daraja.
Comments
Post a Comment