CAPTAIN WA GULIONI AWA MZANZIBAR MWENGINE KUSAJILIWA LIGI KUU BARA
Timu ya Stand United kutoka mkoani Shinyanga imemsajili beki
wa kati ambae ni nahodha wa timu ya Gulioni Ali Hamad Ali “Kinibu” akitokea
kwenye ligi daraja la pili wilaya ya mjini Unguja.
Kinibu amesajiliwa kwenye kikosi hicho cha wapiga debe wa
Shinyanga kwaajili ya kuongeza nguvu msimu ujao wa mashindano yakiwemo kombe la
FA pamoja na ligi kuu soka Tanzania bara.
Mara baada ya kusaini miaka 2 kuitumikia timu hiyo Kinibu
amefurahishwa mno na kusema malengo yake ni kucheza nje ya Tanzania hivyo
ataendelea kupambana ili atimize ndoto
zake.
“Nimefurahi kusaini mkataba wa miaka 2 Stand United, malengo
yangu ni kucheza nje ya Tanzania ntaendelea kujituma ili nitimize ndoto zangu”.
Alisema Kinibu.
Kinibu anavutiwa zaidi na uchezaji wa mlinzi wa kati wa klabu
ya Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa Laurent Koscielny pamoja na mlinzi wa
Spain Sergio Ramos.
Comments
Post a Comment