CAPTAIN WA TAIFA JANG’OMBE SALULA AZUNGUMZIA SABABU YA KUFANYA VIBAYA TIMU YAKE
Ahmed Ali Suleiman “Salula” |
Mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Jang’ombe ambae
pia ni nahodha wa timu hiyo Ahmed Ali Suleiman “Salula” amesema wao wachezaji
hawana tatizo lolote mpaka sasa licha ya kucheza michezo 8 bila ya kupata
ushindi hata mchezo mmoja.
Salula amesema wanapigana kadri ya uwezo wao lakini
anashangaa wanapata matokeo mabaya hivyo amewaomba Mashabiki wao waendelee
kuwaunga mkono katika kipindi hichi kigumu kwani wao wanajitahidi kwa nguvu
zote kupeleka furaha Taifa.
“Sisi tunajishangaa sana, makocha wetu wanatufundisha vizuri
kila siku na tukifika uwanjani tunapata nafasi nyingi sisi kuliko mpinzani wetu
lakini utashangaa mwisho wa mchezo tunafungwa sisi au tunatoka sare, sisi
wachezaji tushakaa pamoja na kujiuliza tuna tatizo gani lakini tunakosa jibu,
hivyo nawaomba mashabiki wetu waendelee kuwa na sisi katika shida na raha na
zaidi tutajipanga kwa msimu ujao mpya”. Alisema Salula.
Katika hatua ya 8 bora ligi kuu soka ya Zanzibar timu ya
Taifa ya Jang’ombe ndio timu pekee ambayo haijawahi kushinda hata mchezo mmoja
katika michezo 8 iliyocheza baada ya kufungwa michezo 5 na kutoka sare michezo
3 wakiwa na alama 3 pekee ambapo mchezo unaofuata Taifa ya Jang’ombe watacheza
na ndugu zao Jang’ombe Boys mchezo ambao utapigwa Jumapili ya July 30, 2017 saa
10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.
Kikosi cha Taifa ya Jang'ombe |
Comments
Post a Comment