DABI ILOKUTANA MARA NYINGI DUNIANI NDANI YA MSIMU MMOJA NI DABI YA JANG’OMBE KATI YA TAIFA NA BOY
Kikosi cha Taifa ya Jang'ombe |
Dabi ya Jang’ombe kati ya Taifa ya Jang’ombe na Jang’ombe
Boys ndio dabi inayoongoza kukutana mara nyingi msimu mmoja kuliko dabi zote
Dunia nzima.
Msimu huu dabi hii mpaka sasa ishakutana mara 5 na kesho
kutwa Jumapili ya July 30, 2017 watakutana tena kwa mara ya 6, hii haijawahi
kutokea Dabi yoyote Duniani kukutana mara 6 ndani ya msimu mmoja.
Kila mji kuna kuwa na dabi mfano pale Jijini Dar es salam
Kariakoo kuna dabi ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga, au kule London Uengereza
kuna dabi ya London kati ya Arsenal na Totenham Spurs, au kule Jijini
Manchester Uengereza kuna dabi ya Manchester kati ya Manchester City na
Machester United, au kule Spain kuna dabi ya Madrid kati ya Atletico Madrid na
Real Madrid, lakini dabi zote hizo kwa msimu mmoja zinakutana mara 2, 3 au 4,
ila kwa dabi ya Jang’ombe itakuwa imevunja rikodi dabi ya kwanza kukutana mara
nyingi msimu mmoja.
Ndani ya msimu huu wa mwaka 2016-2017 ambao kwa Zanzibar bado
unaendelea dabi hiyo walikutana Novemba 19, 2016 katika Bonanza la Coconut FM ambapo
matokeo Taifa 2-0 Boys huku mabao ya Taifa yalifungwa na Mkongo Baraka Ushindi
na Mkenya Mohd Said “Mess.
Disemba 10, 2016 walikutana tena kwenye Ligi kuu soka ya
Zanzibar Mzunguko wa kwanza na mataokeo Taifa 2-2 Boys ambapo mabao ya Taifa
siku hiyo alifunga Omar Yussuf Chande dakika 9 na Abdallah Mudhihir (Mido)
dakika 60 wakati mabao ya Boys yote alifunga Khamis Mussa (Rais) dakika ya 45
na 53.
Disemba 30, 2016 pia walikutana tena kwenye Kombe la
Mapinduzi 2017 na matokeo Taifa 1-0 Boys kwa bao pekee lililofungwa na Hassan
Seif “Banda”.
Aprli 25, 2017 walikutana tena kwenye ligi kuu soka ya
Zanzibar Mzunguko wa pili na matokeo Taifa 0-1 Boys kwa bao pekee limefungwa na
Khamis Mussa “Rais”.
Mei 14, 2017 walikutana tena kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar
hatua ya 8 bora Mzunguko wa kwanza na matokeo Taifa 0-3 Boys ambapo mabao ya
Boys yalifungwa na Khamis Mussa “Rais”, Khatib Ng’ombe alijifunga mwenyewe na Juma
Mess la tatu.
Na kesho kutwa Jumapili ya July 30, 2017 saa 10:00 za jioni
kwenye mzunguko wa pili ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora na huu
utakuwa mchezo wao wa sita kukutana katika msimu mmoja.
Comments
Post a Comment