JKU NA ZIMAMOTO HAKUNA MBABE, JAMHURI YAPATA USHINDI MNENE, KESHO TAIFA NA BOYS
Mzunguko wa 9 wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora
umeanza jioni ya leo kwa kupigwa michezo 2 katika viwanja 2 tofauti.
Katika uwanja wa Amaan kisiwani Unguja timu ya JKU na
Zimamoto wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 1-1.
Bao la Zimamoto limefungwa na Ibrahim Hamad Hilika dakika ya 15
wakati bao la JKU limefungwa na Is haka Othman “Bopa” dakika ya 81.
Nako huko katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba, timu ya
Jamhuri imeondoka na alama 3 muhimu baada ya kushinda mabao 5-3 dhidi ya
Mwenge.
Mabao ya Jamhuri yamefungwa na Mwalimu Mohammed (Hat trick) dakika
ya 11, 15, 27, Khamis Abrahman “Mburu” dakika ya 60, na Mussa Ali Mbarouk
dakika ya 88 ambapo mabao ya Mwenge yote matatu (Hat trick) yamefungwa na
Abdull Yussuf dakika ya 33, 37 na 79.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho saa 10:00 za jioni kwa
kupigwa mchezo kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Jang’ombe Boys kwenye uwanja
wa Amaan na katika uwanja wa Gombani watasukumana kati ya Okapi dhidi ya
Kizimbani.
Comments
Post a Comment