MADUNDO APANIA KUPANDA TENA DARAJA TIMU YAKE YA VILLA UNITED
Baada ya kufanikiwa kupanda daraja la kwanza Taifa msimu
ulopita Timu ya Villa United “Mpira Pesa” yenye Maskani yake Mwanakwerekwe
imepania na msimu huu mpya kuondoka daraja hilo na kupanda daraja jengine.
Akizungumza na Mtandao huu kocha mkuu wa timu hiyo Ramadhan
Abdulrahman “Madundo” amesema kwa soka la Zanzibar lilivo hawana sababu timu
yao isipande tena daraja msimu huu kama ilivyofanya miaka miwili mfululizo
iliyopita.
“Sisi kila mwaka tunapanda daraja jengine sasa sioni sababu
na mwaka huu tusipande daraja jengine, kwani nina wachezaji wenye uwezo binafsi
na pia uongozi wangu upo imara”. Alisema Madundo.
Timu ya Villa United ilianzishwa mwaka 2013 ambapo ilianzia
kucheza madaraja ya Vijana Wilaya ya Mjini lakini ilipofika msimu wa mwaka
2015-2016 ilishiriki ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini na kufanikiwa kupanda
daraja, Msimu ulopita wa mwaka 2016-2017 Villa ilifanikiwa tena kupanda daraja la
Kwanza Taifa ambapo msimu ujao mpya wa mwaka 2017-2018 pia wamepania kupanda
daraja jengine kama ni ligi 2 au ligi kuu soka ya Zanzibar itategemea msimu huu
mfumo gani utatumika kwenye madaraja husika.
Comments
Post a Comment