TAIFA YA JANG'OMBE BADO IPO ICU, MECHI YA 8 BILA YA USHINDI
Timu ya Taifa ya Jang'ombe imeendelea kuvuruga katika ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora baada ya jioni ya leo kukubali kuchapwa mabao 2-0 na JKU, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Amaan.
Mabao ya JKU yamefungwa na Mbarouk Chande dakika ya 58 na Amour Omar "Janja" dakika ya 64.
Nako huko katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba timu ya Kizimbani imeichapa Mwenge bao 1-0.
Bao la Kizimbani limefungwa na Ali Mkadam dakika ya 68.
Ligi hiyo itaendelea Jumamosi.
Zimamoto v/s JKU, Amaan.
Jamhuri v/s Mwenge, Gombani.
Jumapili
Okapi v/s Kizimbani, Gombani.
Jang'ombe boys v/s Taifa ya Jang'ombe
Mechi zote hizo saa 10:00 za jioni.
Comments
Post a Comment