TAIFA YAENDELEZA UTEJA KWA BOYS, YAPIGWA MARA 3 MFULULIZO
Timu ya Jang'ombe boys imeendeleza wimbi lake la ushindi mbele ya kaka zao Taifa ya Jang'ombe baada ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Amaan.
Mabao ya Boys yamefungwa na Hafidh Barik (Fii) dakika ya 6 na Juma Ali (Mess) dakika ya 66.
Nako huko katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba timu ya Kizimbani wakaichapa Okapi mabao 2-1.
Mabao ya Kizimbani yamefungwa na Khamis Suleiman dakika ya 49 na Haji Rashid dakika 62 wakati bao pekee Okapi limefungwa na Seif Saleh dakika ya 90.
Comments
Post a Comment