TIMU 4 ZILIZOPANGA MATOKEO 11-1, 7-1 CENTRAL WILAYA YA MJINI ZAPIGWA FAINI NA KUFUTWA KATIKA MASHINDANO, VIONGOZI WA TIMU HIZO WOTE WAFUNGIWA MWAKA MMOJA
Kikosi cha FC Muembe beni |
Kamati ya Soka la Vijana Wilaya ya Mjini imezipiga faini ya
jumla ya shilingi laki tatu na kuziondosha katika Mashindano timu za FC Muembe
beni, Real Kids, Schalke 04 na King Boys baada ya kukutwa na hatia ya upangaji
wa matokeo katika mechi zao za mwisho za hatua ya 4 bora zilizopigwa Jumapili
iliyopita ya July 23, 2017.
Katika michezo hiyo miwili iliyovikutanisha vilabu hivyo vinne,
michezo ambayo ilikuwa inatafuta Bingwa wa Daraja hilo la Central ambapo timu
ya Schalke 04 ilishinda
mabao 11-1 dhidi ya King Boys wakati mchezo mwengine FC Muembe beni iliwafunga Real
Kids 7-1 ndipo hapo baada ya kumalizika michezo hiyo viongozi wa Mashindano
hayo wakashindwa kutoa zawadi na kupelekea jana kutoa maamuzi hayo baada ya
kamati kujiridhisha.
Khamis Machano ambae ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema wametoa
maamuzi hayo kwakuwa wamejiridhisha kwamba timu hizo zimepanga matokeo na kuamua
kuzifuta na pamoja na kuzipiga faini ya shilingi laki tatu.
“Kamati tumekaa na kuamua kuwapiga faini ya shilingi laki
tatu kwa kila timu kati ya hizo nne mana kuna kila sababu ya kuwa wamepanga
matokeo, baada ya kupitia ripoti za makamisaa zinaeleza kuwa michezo hiyo ina
viashiria vya upangaji wa matokeo, kwa mujibu wa kanuni zetu kifungu nambari 25
kinatuamuru kuzifuta timu zote na kuzipiga faini ya shilingi laki tatu kutokana
na kitendo hicho”.
Wakati huo huo Kamati hiyo imewafungia mwaka mmoja
kutojihusisha na soka viongozi wote wa timu hizo nne ambao walikaa kwenye
Mabenchi kwenye michezo hiyo.
“Viongozi wote waliyokaa kwenye Mabenchi kwenye michezo hiyo
tumewafungia mwaka mmoja kutojihusisha na soka”. Alisema Machano.
Kikosi cha Real Kids |
Comments
Post a Comment