GULIONI YAANZA KWA KISHINDO WILAYA YA MJINI
Timu
ya Soka ya Gulioni FC imeanza vyema ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini baada
ya kuitandika Dira FC mabao 5-0 kwenye mchezo uliopigwa saa 8 za mchana katika
uwanja wa Amaan.
Mabao
ya Gulioni yamefungwa na Maulid Salum Abdallah akipiga Hat trick dakika ya 14,
48 na 88 huku mabao mengine yakifungwa na Haji Juma Ali dakika ya 22 na 24.
Ligi
hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.
Saa
8:00 za mchana wataanza Shangani dhidi ya Gereji, na saa 10:00 za jioni
watasukumana kati ya Kundemba dhidi ya Muembe Makumbi.
Comments
Post a Comment