SHANGANI NA MUEMBE MAKUMBI ZANGARA WILAYA YA MJINI
Timu ya Shangani na Muembe Makumbi zimeanza vyema ligi daraja
la Pili Wilaya ya Mjini baada ya kushinda michezo yao ya leo kwenye uwanja wa
Amaan.
Saa 10 za jioni Shangani waliichapa Gereji 2-0 kwa mabao
yaliyofungwa na Abdallah Maulid dakika ya 42 na Pesto Is-haka dakika ya 45.
Saa 8 za mchana Muembe Makumbi wakaichapa Kundemba bao 1-0
kwa bao pekee lililofungwa na Ame Ibrahim Mohammed dakika ya 76.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili
katika uwanja wa Amaan.
Comments
Post a Comment