TAIFA YA JANGOMBE YAREJEA ZANZIBAR WAKITOKEA KAMBI TANGA
Timu ya Taifa ya Jang’ombe wamerejea Visiwani Zanzibar jioni ya leo wakitokea mkoani Tanga ambapo waliweka kambi ya wiki mbili.
Mara baada ya kuwasili tu Unguja Taifa wakaenda kumjulia hali
mdhamini wao mkuu Salim Hassan Turkey huko Mpendae Mjini Unguja.
Turkey ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Mpendae amefurahishwa
mno kutembelewa na vijana wake ambapo pia amesema wakitwaa ubingwa wa ligi kuu
soka ya Zanzibar msimu huu atawafanyia jambo kubwa wachezaji hao.
“Nawapongeza kwa kuja kunijuulia hali, ahsanteni wachezaji
wangu, mwaka jana niliahidi mukichukua ubingwa ntakupelekeni China kukaa kambi,
lakini kwa bahati mbaya hatukuchukua ubingwa ndo mana tukaenda kambi Tanzania
bara, lakini msimu huu ntaangalia mechi mbili kasha ntakupeni ahadi nzito”.
Alisema Turkey.
Wakati huo huo kocha mkuu wa Taifa ya Jang’ombe Saleh Juma
Maisara amesema kambi yao ilikuwa nzuri sana na imewasaidia kujijenga vizuri
zaidi kwenye ligi kuu ambapo kwasasa kikosi chake kipo tayari kupambana.
“Kambi yetu ilikuwa ni ya wiki mbili, nashkuru tulilolitafuta
tumelipata, vijana wapo vizuri sana naamini sasa wapo tayari kupambana”.
Alisema Maisara.
Mwisho timu hiyo kwa pamoja wakapiga kisomo kizito
kilichoongozwa na nahodha wao Ahmed Ali Salula, dua ambayo ni ya kumuombea
Mdhamini wao pamoja na kuifanya vyema timu hiyo.
Mchezo
wake wa kwanza Taifa ya Jang’ombe itacheza dhidi ya Zimamoto
mchezo ambao utapigwa Oktoba 5 mwaka huu saa 8:00 za mchana katika uwanja wa
Amaan.
Comments
Post a Comment