TEDDY: WAAMUZI ZANZIBAR WATALIPWA KABISA KABLA YA KAZI

Waamuzi watakaochezesha Mashindano yanayosimamiwa na ZFA Taifa wameahidiwa kulipwa pesa zao kabisa kabla ya kuanza kwa ligi ili kuepusha kutowajibika kikamilifu.

Ameyathibitisha Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar Mohammed Ali Hilali (Teddy) ambapo amesema msimu huu watawalipa waamuzi kabisa kabla ya kuanza kwa ligi ili wazidi kusimamia vyema sheria 17 za soka.

“Nahakikisha baada ya siku nne kutoka leo (Jana) pesa za Waamuzi zote za msimu huu ntamkabidhi Mwenyekiti wa kamati ya Waamuzi, hatutaki kudaiwa tena msimu huu, tutawapa chao kabisa ili tuwadai wao mechi na si kutudai sisi". Alisema Teddy.

Ligi kuu soka visiwani Zanzibar inatarajiwa kuanza Jumanne ya Oktoba 3, mwaka huu ambapo mechi za awali ni Mafunzo Vs JKU saa 8:00 mchana
kisha Jang'ombe Boys Vs KMKM saa 10:00 jioni katika uwanja wa Amaan.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA