AZIZ SHAWEJI ASIMAMISHWA MECHI 4 KUCHEZA LIGI KUU ZENJ NA KOCHA ABRAHMAN MUSSA NAE APIGWA STOP KUKAA KATIKA BENCHI
Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kimempa
adhabu ya kumsimamisha kucheza mechi nne beki wa Kilimani City, Aziz Shaweji
baada kupatikana na hatia ya kukiuka nidhamu ya michezo katika mechi kati ya
Kilimani City na Black Sailors iliyopigwa juzi Jumapili saa 8 za mchana katika
uwanja wa Amaan.
Akizungumzia kadhia hiyo katibu
mkuu wa ZFA Mohd Ali Hilali “Tedy” amesema Shaweji alipatikana na kosa wakati
timu yake ya Kilimani City ilipofungwa 2-0 na Black Sailors ambapo alimzonga Muamuzi
wa kati wa mchezo huo Mfaume Ali Nassor.
Hivyo Shaweji atazikosa mechi kati
ya Kilimani City dhidi ya Jang’ombe Boys itakayopigwa Oktoba 30, Kilimani city
na Chuoni ya Novemba 6, Kilimani city dhidi ya Charawe ya Novemba 12 na ya
mwisho Kilimani city dhidi ya Zimamoto itakayopigwa Novemba 19.
Wakati huo huo kocha wa
Kilimani City Abrahman Mussa nae
amesimamishwa kukaa katika benchi hadi pale atakapopeleka vyeti vyake vya
ukocha ZFA.
Katibu Tedy amesema wamemsimamisha mpaka wathibitishe cheti chake cha
ukocha kama kweli anastahiki kuwa Mwalimu wa Soka kwani katika mchezo kati Kilimani
City walipochapwa 2-0 na Black Sailors uliyopigwa juzi Jumapili saa 8 za mchana
katika uwanja wa Amaan Mwalimu huyo baada ya kumaliza mchezo alimzonga Muamuzi wa
kati wa mchezo huo Mfaume Ali Nassor.
Comments
Post a Comment