BOYS KAMA TAIFA, YABANWA NA CHUONI LEO
Mzunguko wa tatu wa ligi kuu soka Zanzibar Kanda ya Unguja umehitimishwa
jioni ya leo kwa kupigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Amaan kati ya Jang’ombe
Boys na Chuoni ambao wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya 0-0.
Kwa matokeo hayo Boys amefikisha alama 2 baada ya kucheza
michezo mitatu kwa kwenda sare miwili na kufungwa mmoja wakati Chuoni
amejikusanyia alama 4 baada ya kushinda mmoja, sare mmoja na kufungwa mmoja.
Mzunguko wa nne wa ligi hiyo utaanza Ijumaa Oktoba 27 katika
uwanja wa Amaan saa 10:00 za jioni Miembeni City dhidi ya Chuoni .
Comments
Post a Comment