MAKOCHA WA SOKA MAGHARIBI B WAANZA KUPIGWA MSASA
Chama
cha Soka Zanzibar (ZFA) leo kimefungua kozi ya makocha wa mpira wa miguu kwa ngazi
ya awali (Priminary) kozi ambayo imefanyika katika Ukumbi wa ZFA
Wilaya ya Magharibi B Mwanakwerekwe Ijitimai.
Akifungua kozi hiyo Makamo wa Urais wa ZFA Unguja Mzee Zam Ali amewapongeza ZFA Wilaya ya Magharibi B kwa kuandaa kozi hiyo na amewataka washiriki kuendelea kujifunza zaidi ili Zanzibar watowe makocha bora.
“Nawapongeza ZFA Wilaya ya Magharibi B kwa kuandaa kozi hii nawapongeza
sana, tena mukimaliza hii muendeleze tena kusoma mkufunzi bi Nassra ni hodari
sana tunampongeza, nimefurahi washiriki wanatoa Wilaya tofauti na wengine mpaka
Pemba nimefurahi sana nategemea tutatoa makocha bora”. Alisema Zam.
Nae mkufunzi wa kozi hiyo Nassra Juma ambae anatambulika Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) amesema kupitia kozi hiyo yatatokea mabadiliko makubwa na kuibuka makocha wazuri ambao watalisaidia soka la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

“Kama
watakuwa wasikivu katika masomo yao, naamini makocha hawa watalisaidia soka la
Zanzibar na Tanzania kwa ujumla”.
Jumla
ya Makocha 31 kutoka Wilaya mbali mbali
wameingia katika Kozi hiyo ya siku 10 ambayo watafundishwa kwa nadharia
na vitendo, kozi ambayo imeandaliwa na Chama cha Soka Wilaya ya Magharibi B.
Comments
Post a Comment