MIEMBENI CITY MECHI NNE SAWA NA DAKIKA 360 BILA YA GOLI, KESHO TAIFA NA JKU HAPATOSHI
Ligi kuu
soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja imeendelea tena leo kwa kupigwa mchezo mmoja
katika uwanja wa Amaan majira ya saa 10 za jioni ambapo Miembeni City wakatoka
sare ya 0-0 na Chuoni.
Kwa matokeo
hayo Chuoni inajikusanyia alama 5 baada ya kushinda mmoja, sare miwili na kufungwa
mmoja wakati Miembeni city wana alama moja kufutia kufungwa mitatu na sare
mmoja wa leo.
City walianza kufungwa na Polisi 1-0, wakachapwa 1-0 na
Mafunzo, kisha kupigwa 1-0 na JKU na leo kutoka sare ya 0-0 na Chuoni, hivyo
wamecheza dakika 360 pasipo kutingisha nyavu za wapinzani hata mara moja.
Ligi hiyo
itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo
saa 8:00 za mchana Taifa ya Jang’ombe dhidi ya JKU na Saa 10:00 za jioni KVZ na
Mafunzo.
Comments
Post a Comment