SIMBA WAMALIZA KAMBI ZANZIBAR NA KUREJEA NYUMBANI DAR KWA NDEGE LEO ASUBUHI
Kikosi cha Simba kimeondoka Visiwani Zanzibar leo saa 3 za
asubuhi kwa Ndege na kurejea jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho ya
mechi yao ya kesho ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Yanga kwenye uwanja
wa Uhuru.
Akizungumza na Mtandao huu wakati waondoka
hapa Zanzibar kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Afisa
Habari wa Simba Haji Manara amesema akili yao yote ni kuifunga Yanga kesho
kwenye uwanja wa Uhuru huku akiwataka Mashabiki wa Simba waendelee kuishangiria
timu yao.
“Kambi ya Zanzibar ilikuwa nzuri sana naamini tumefikia
malengo yetu, hapa tunaondoka na leo jioni Dar tutafanya mazoezi ya mwisho,
nawaomba Mashabiki wa Simba wazidi kuishangiria timu yao”. Alisema Manara.
Simba walikuwa kambini mjini hapa tangu Jumatatu ya Oktoba 23 na
leo Ijumaa Oktoba 27 wamerejea nyumbani Dar es salam kuwavaa Yanga.
Comments
Post a Comment