TAIFA YA JANG’OMBE MAMBO BADO MECHI NNE HAWAJAONJA LADHA YA USHINDI, KVZ NA MAFUNZO WALA SAHANI MOJA, KESHO KMKM NA ZIMAMOTO
Timu ya Taifa ya Jang’ombe (Wakombozi wa Ngambo) imeendelea
kucheza pasipo kupata ushindi katika michezo yake ya ligi kuu soka ya Zanzibar
kanda ya Unguja baada ya leo saa 8 za mchana kutoka sare ya 0-0 dhidi ya JKU katika uwanja wa Amaan.
Kwa matokeo hayo Taifa imefikisha alama 3 kufuatia kufungwa
mchezo mmoja na kutoka sare michezo mitatu wakati JKU amejikusanyia alama 10
baada ya kushinda michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja.
Saa 10 za jioni ulipigwa mchezo mwengine katika uwanja wa
Amaan kati ya KVZ na Mafunzo mchezo ambao umemalizika kwa sare ya 0-0.
KVZ anaongoza ligi hiyo akifuatiwa na JKU baada ya timu zote
hizo kuwa na alama 10 katika michezo yao 4 waliyocheza huku Mafunzo baada ya
mechi ya leo amefikisha alama 5 kufutia kushinda mmoja, sare 2 na kufungwa
mmoja.
Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja itaendelea tena
kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.
Saa 8:00 za mchana wataanza Wana Jeshi timu ya Kipanga
kukupiga na Maafande wa Polisi na saa 10:00 za jioni watachuwana kati ya KMKM
dhidi ya Zimamoto.
Zimamoto |
MissoQstup_be_Wilmington Natalie White https://wakelet.com/wake/FW0fg3FgSDZy5i_KfNHkk
ReplyDeletefidniginnoa
Ytinccidest-zo Sarah Marie click here
ReplyDeletelink
download
click
izicprogun