BLACK SAILORS YAKAA KILELENI LIGI KUU ZENJ, YAIGONGA MAFUNZO

Timu ya Black Sailors (Mabaharia Weusi), imefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja baada ya kuichapa Mafunzo bao 1-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan jioni ya leo.

Sailors imekaa kileleni baada ya kufikisha jumla ya ponti 15 ilizozipata baada ya kushinda mechi tano na kupoteza miwili,itakuwa sawa na JKU ambayo nayo ina alama 15 baada ya kuichapa KMKM mchana wa leo ambapo Sailors anaongoza akiwa na mabao mengi zaidi ya JKU.

Bao pekee la Sailors limefungwa na Malik Haji katika dakika ya 25.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo Saa 8:00 za mchana Polisi watakuwa na kazi ya kucheza na Jang'ombe Boys na saa 10:00 za jioni Kilimani city watakipiga na Zimamoto.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA