FAINALI YA MASHINDANO YA MAJIMBO KUPIGWA KESHO, ZAWADI YA GARI IPO KWAAJILI YA BINGWA
Fainali ya Soka ya Mashindano ya Majimbo ya Unguja inatarajiwa
kupigwa kesho Jumamosi ya Novemba 25 kati ya timu ya Jimbo la Kwahani dhidi ya
Afisi Kuu ya CCM kwenye uwanja wa Amaan majira ya saa 10:00 za jioni.
Mapema saa 8:00 za mchana siku hiyo kutaanza
kutafutwa mshindi wa tatu ambapo watacheza Jimbo la Malindi dhidi ya Kikwajuni.
Uledi Said ambae ni Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano hayo amesema Bingwa atazawadiwa Gari aina ya Carry, medali za dhahabu pamoja na Kombe huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano
Tanzania Kassim Majaaliwa .
Comments
Post a Comment